Mwenyekiti wa Bodi ya Rufani ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (AAAB) Jaji Mstaafu. Sirillius Matupa amewaasa watendaji wa Bodi hiyo kuwa waadilifu wakati wa kutatua Rufaa za wadau wao. Hayo ameyasema wakati akisoma Hotuba yake mbele ya mgeni rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo.