HUDUMA ZA RUFAA
UTARATIBU WA KUKATA RUFAA
Rufaa itawasilishwa kwa kufuata utaratibu ufuatao:
- Kuwasilisha Notisi ya Rufaa ndani ya siku 30 tangu tarehe ambayo uamuzi ulitolewa.
- Kufungua rasmi rufaa ndani ya siku 21 tangu tarehe ya kuwasilisha Notisi ya Rufaa.
NYARAKA ZA RUFAA
Rufaa itafunguliwa kwa kuwasilisha kwa Msajili nyaraka zifuatazo:
- Nakala ya Hati ya Sababu za Rufaa (Memorandum of Appeal).
- Nakala ya Kumbukumbu za Rufaa (Record of Appeal).
ADA ZA RUFAA
|
Na. |
Maelezo |
Mtu Binafsi (TSh) |
Kampuni (TSh) |
|---|---|---|---|
|
1 |
Ada zinazohusu Rufaa |
||
|
Kuwasilisha Notisi ya Rufaa |
30,000 |
50,000 |
|
|
Kuwasilisha Kumbukumbu za Rufaa na Hati ya Sababu za Rufaa |
200,000 |
500,000 |
|
|
2 |
Ada zinazohusu Maombi |
||
|
Kuwasilisha Chamber Summons pamoja na Hati ya Kiapo (Affidavit) au Hati ya Kiapo cha Majibu (Counter Affidavit) |
30,000 |
50,000 |
|
|
3 |
Ada zinazohusu Mashauri ya Kuingilia Rufaa (Intervention Proceedings) |
||
|
Kuwasilisha Notisi ya Kuingilia Shauri |
30,000 |
50,000 |
|
|
Kuwasilisha Taarifa ya Kuingilia Shauri |
30,000 |
50,000 |
|
|
Kuwasilisha Majibu kwa Taarifa ya Kuingilia Shauri |
30,000 |
50,000 |
|
|
4 |
Ada zinazohusu Uwasilishaji wa Nyaraka |
||
|
Kuwasilisha nyaraka nyingine yoyote |
20,000 |
30,000 |
|
|
5 |
Huduma Nyingine |
||
|
Kupata nakala ya uamuzi wa Bodi ya Rufani |
20,000 |
30,000 |
|
|
Kukagua jalada la shauri |
20,000 |
30,000 |